MBARONI KWA KUMUUA MGANGA WAKIJARIBU DAWA ZA KUZUIA RISASI
Kijana akamatwa kwa kumuua mganga wa kienyeji wakijaribu dawa ya kuzuia risasi. Raia mmoja wa nchini Nigeria ajulikanaye kwa jina la Chukwudi Ijezie amekamatwa na jeshi la polisi kwa kumuua mganga wa
kienyeji katika kijiji kimoja nchini humo kwa kutumia bunduki.
Kijana huyo alijikuta katika hatima hiyo ya mauji pasipo kukusudia baada ya kuambiwa na mganga huyo kwamba ana dawa yenye uwezo wa kuzuia risasi na kumtengenezea kijana huyo dawa hiyo na kisha kumuambia aifunge shingoni na baada ya kijana huyo Chukwudi kuonyesha kutokumuamini ndipo mganga huyo alipomkabizi bunduki hiyo na kisha kuvaa dawa ile shingoni mwake kumwambia ajaribu kumpiga bunduki hiyo ili aone uwezo wa dawa hiyo. Naye alipofanya alichoagizwa na mganga huyo basi matokeo yaka yakawa kinyume na matarajio yao.
Mganga huyo aliyefahamika kwa jina Chinaka Adoezuwe mwenye umri wa miaka 26 ndipo alianguka chini na kuanza kutapatapa kisha kufariki wakati akikimbizwa hospitali kwa msaada wa matibabu.
Hata hivyo wakazi wa maeneo hayo wamedai kuwa wapo waganga kadhaa katika maeneo yao wanaojitapa na kutengeneza dawa zinazodhibiti kupatwa na risasi unapopigwa, na kudai kwamba watu kutoka maeneo ya mbali huja kwa ajili ya dawa hizo
Sunday, July 15, 2018