Kazi ya kuhesabu kura kuendelea vizuri nchini TANZANIA
Kazi ya kuhesabu kura imeanza nchini Tanzania baada ya siku nzima ya upigaji kura Jumapili. Mamillioni ya watu kote nchini walijitokeza kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha kuchagua marais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, pamoja na wabunge, wawakilishi, madiwani na masheha.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva, amesema katika matangazo ya moja kwa moja kuwa ana imani kuwa uchaguzi huyo utaonekana kuwa wa haki na wa wazi licha ya matatizo ya hapa na pale katika vituo.
Hata hivyo, sehemu kubwa ya ripoti kutoka kwa waandishi katika maeneo mbali mbali nchini zimesema upigaji kura ulienda salama bila usumbufu katika vituo vingi vya upigaji kura.
Mgombea wa chama tawala CCM, John Magufuli. alipiga kura katika wilaya yake ya uchaguzi Chato katika mkoa wa Mwanza, wakati mgombea wa upinzani, Edward Lowasa, alipiga kura nyumbani kwake Monduli.
Nao wagombea urais Zanzibar, Rais wa sasa Ali Mohamed Shein wa CCM na mpinzani wake Seif Shariff Hamad wa chama cha CUF walikuwa miongoni mwa watu kwanza kujitokeza mjini Unguja kupiga kura zao.
Kulingana na tume ya uchaguzi matokeo ya kura kwa upande wa wabunge na madiwani yataanza kujulikana ifikapo usiku wa manane kwa saa za Afrika Mashariki. Matokeo ya uchaguzi wa rais yatatangazwa rasmi Oktoba 28 lakini tume imesema huenda pia yakajulikana saa 48 baada ya upigaji kura kufungwa.
katika matukio haya ya kuhesabu kura na waangalizi wakimataifa hawakombali
PICHA CHAFU ZA WANAFUNZI WAKIFANYA UCHAFU ZAVUJA FACEBOOK SEE PHOTOS BELOW =>AdvertisementKAMA HUJAONAILE VIDEO CHAFU YA ZARI THE BOSS LADY ILIYOVUJA BOFYA HAPO CHINI=> Advertisement
Post a Comment