Wanafunzi 65 Kuondoka kwa Masomo Nchini China.
Sehemu
ya wazazi na wanafunzi wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya
juu wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL),
Abdulmaalik Mollel (hayupo pichani) wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akitoa
nyaraka za taarifa za wanafunzi wanaokwenda nchini China wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiuliza swali kwa masomo wanayokwenda kusoma katika vyuo vya nje wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza
na mzazi wa mwanafunzi wa anyekwenda kusoma nchini China wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Mollel
amesema vyuo vya nje ambavyo vinashirikiana na GEL vina ubora wa elimu
pamoja na kuwa na vitendea kazi vinavyoweza kufanya mwanafunzi afanye
vizuri katika masomo yao.
Amesema wanafunzi 500, GEL imesha wadahili katika vyuo vya nje na
wanafunzi hao wameona ubora wa vyuo hivyo na kuweza kuleta chachu ya
maendeleo nchini kutokana na utaalam wataopata huko.
Mollel
amesema kuwa nafasi bado zipo katika vyuo vya China hivyo wazazi
wanaweza kuwasiliana na GEL kufanya usajili katika vyuo hivyo.
“Nia ya GEL ni kuona wanafunzi wanafanya vizuri katika matokea na
tunafatilia tabia zao hatua kwa hatua tukiwa na lengo ya kupata wasomi
wenye ujuzi kwa maendeleo ya taifa”amesema Mollel.
Aidha
amesema kuwa wanafunzi wanaonyesha tabia mbaya wanawarudisha nchini
katika kuweza kuokoa fedha za mzazi kuendelea kuhudumia mtoto ambaye
mwishoni hatafanya vizuri.
Post a Comment