MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI WALETA MAAFA KATIKA KIJIJI CHA DIHINDA MVOMERO MKOANI MOROGORO,WAZIRI WA KILIMO,UVUVI NA UFUGAJI MWIGULU NCHEMBA ATEMBELEA KUJIONEA
Waziri
wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akiangalia Ng'ombe walio
uwawa katika Mgogoro wa wakulima na Wafugaji katika kijiji cha Dihinda
kata ya Kanga wilayani Mvomero, katika tukio lililotokea Desemba 12
mwaka huu
Waziri
wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya
ya Mvomero, Beth Mkwasa wakiwajulia hali watu waliojeruhiwa katika
mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu.

Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akizungumza na Mkuu wa wilaya Mvomero, Beth Mkwasa katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12
mwaka huu, walipotembelea katika kijiji hicho na kuona madhara makubwa
yaliyojitokeza katika mgogoro wa wakulima na wafugaji. Nchemba
alimwagiza Mkuu wa wilaya Mvomero, Beth Mkwasa kuunda
kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya ya Mvomero ili kamati ihusike
maeneo yote ya Nchi yetu ili kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo yote
yenye migogoro, pia wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara
moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.

Waziri
wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akizungumza wanachi wa
kijiji cha Dihinda waliokusanyika katika eneo lililotokea mauaji ya
wanyama na baadhi ya watu kujeruhiwa.
"Natoa
rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, kuwa hakuna
ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule,
njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na
wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa Serikali wa eneo
husika hatua kwa hatua, Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria
mikononi, t
unakwenda
kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji
zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na
kuwachukulia hatua za kisheria."
Alisema Nchemba.
Post a Comment