SHAMBULIZI LA KIGAIDI KATIKA MAKAZI YA RAIS SOMALIA LAUWA WATU 20
Bomu hilo lililotegwa kwenye gari lililipuka katika makao ya rais wa Somalia kwenye mji mkuu wa Mogadishu na kuua takriban watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30 siku ya Jumanne. Hayo ni kulingana na maafisa wa usalama nchini Somalia.
Mlinzi mmoja wa rais wa Somalia ambaye hakutaka jina lake litajwe,
amesema kuwa mtu aliyekuwa anaendesha gari kwa kasi
alianza kufyatua risasi na ikabidi walinzi kumfyatulia risasi pia.
Hatimaye dereva huyo alisimamisha gari lake na kulipua bomu
lililokuwemo.
MBUNGE ABDALLA BOSS AMBAYE NAYE NI MAJERUHI |
Post a Comment