BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA WA MTUHUMU MSAJILI WA VYAMA KUANDAA MPANGO HARAMU UTAKAO SABABISHA KUFUTA CHAMA HICHO
Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limetoa pongezi kwa Kamati Kuu ya chama hicho kuahirisha maandamano na mikutano ya nchi nzima iliyopewa jina la Ukuta.
Maandamano
hayo ambayo yalipangwa kufanyika kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu
yaliahirishwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa madai ya kuombwa na
viongozi wakuu wa madhehebu ya dini.
Akizungumza
katika Makao Makuu ya chama hicho jana, Katibu Mkuu wa Baraza hilo,
Roderick Lutembeka alisema, hatua ya kamati hiyo kuahirisha maandamano
hayo ni muhimu na inaonesha jinsi chama hicho kina viongozi wavumilivu.
“Kwa
kutambua moyo wa kiuongozi waliouonesha na dhamira ya dhati ya
kuwatumikia Watanzania wote, tunapenda kuwapongeza viongozi wetu wakuu
kwa uamuzi huu wa busara ambao umeuthibitishia umma kuwa chama kina
viongozi imara,” alisema Lutembeka
“Taarifa
zinaonesha njama hizo zinalenga kukihujumu Chadema kwa kuandaa mitego
haramu ya kisiasa ili hatimaye yatolewe mapendekezo ya kukifuta katika
orodha ya vyama vya siasa,” alisema Lutembeka na kuongeza;
“Tarehe
15 Agosti mwaka huu Jaji Mtungi alitangaza kuwa, Baraza la Vyama vya
Siasa lilikuwa limeitisha kikao ambacho kingefanyika tarehe 29-30 Agosti
kujadili masuala ya hali ya kisiasa nchini. Siku mbili kabla ya kikao
Mwenyekiti wa baraza akatangaza kukiahirisha hadi tarehe 3-4 mwezi huu.
“Wakati
taarifa zote hizo zikitolewa na viongozi wa baraza, ofisini hapa
(Chadema) hakuna hata barua moja kutoka kwa msajili ya kutuita katika
kikao chochote kati ya hivyo. Kuanzia kile cha tarehe 29-30 Agosti,
tarehe 3-4 Septemba wala hiyo ya kuahirisha.
“Katika mazingira haya nani ambaye hatashawishika kuamini ofisi ya msajili inatii maagizo ya watawala,”
Post a Comment