NI BAADA YA KUGOMA KURUDI NCHINI MWAO WALIPOFUNGWA NA BOTSWNA
UMOJAWA MATAIFA WAINGILIA KATI JAMBO HILO
Timu ya Eritrea ilishindwa na Botswana mechi hiyo ya kufuzu Kombe la Dunia
Botswana imewapa
hifadhi wanasoka 10 wa timu ya taifa ya Eritrea waliokataa kurejea
nyumbani baada ya kucheza mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia, wakili wao
amesema.
Dick Barford amesema amejulishwa uamuzi huo na waziri wa haki, ulinzi na usalama wa Botswana Augustine Makgonatsotlhe.Wengi wa wachezaji soka wa Eritrea wamekuwa wakikataa kurejea nyumbani na kuomba hifadhi baada ya kucheza mechi ugenini.
Wachezaji sita waliomba hifadhi Angola mwaka 2007, 12 nchini Kenya mwaka 2009 na wengine 18 nchini Uganda mwaka 2012.
Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloangazia haki za kibinadamu mwezi Juni liliituhumu serikali ya Eritrea kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Mamia ya maelfu ya raia wa Eritrea wamekuwa wakitoroka taifa hilo.
Eritrea imekanusha madai ya kukiuka haki za kibinadamu na kusema wanaoondoka nchini humo ni “wahamiaji wa kiuchumi”. PICHA CHAFU ZA WANAFUNZI WAKIFANYA UCHAFU ZAVUJA FACEBOOK SEE PHOTOS BELOW =>AdvertisementKAMA HUJAONAILE VIDEO CHAFU YA ZARI THE BOSS LADY ILIYOVUJA BOFYA HAPO CHINI=> Advertisement
Post a Comment