YANAYOJIRI KATIKA SIASA LEO
MATUKIO MBALIMBALI YA UCHAGUZI NCHINI TANZANI;
LOWASA KUKATAZWA KUINGIA KATIKA JUMBA LA KUTANGAZIA MATOKEO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza matokeo ya urais ya majimbo 34.
Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania pamoja na Ireland Kaskazini umetoa taarifa ukipinga kufutiliwa mbali kwa matokeo ya Uchaguzi kisiwani Zanzibar.
Ubalozi huo umesema kuwa hauoni sababu za kufutiliwa mbali kwa matokeo hayo ilhali waangalizi walifurahishwa na vile uchaguzi huo ulivyofanyika kwa amani.
Wameitaka tume ya uchaguzi Kiswani Zanzibar kuorodhesha matokeo hayo bila kuchelewa.
Mgombea wa urais wa chama cha CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA Edward Lowassa wameelekea katika makao ya tume ya uchaguzi NEC kuwasilisha pingamizi yao kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu Tanzania. Baada ya kutoka huko wataelekea katika makao makuu ya UKAWA kuvihutubia vyombo vya habari.
Kufikia sasa mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CCM John Pombe Magufuli anaendelea kuongoza katika kura zilizohesabiwa.
Rais mpya wa Tanzania kujulikana leo
Tume ya uchaguzi nchini Tanzania hii leo inatarajiwa kumtangaza rais mpya wa taifa hilo hii leo.Hatua hii inajiri siku moja tu baada ya Upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na udanganyifu mkubwa. Tayari tume ya uchaguzi Kisiwani Zanzibar imefutilia matokeo ya uchaguzi kisiwani humo.
Makamishna wa tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar wameushtumu uamuzi wa mwenyekiti wao Jecha Salum Jecha kwa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa kisiwa hicho bila ya kuwashauri
Tume ya uchaguzi kisiwani Zanzibar inajiandaa kutangaza tarehe mpya ya marudio ya uchaguzi huo.
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu matukio tofauti nchini humo. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza matokeo ya majimbo takriban 187 na matokeo zaidi yanatarajiwa leo. PICHA CHAFU ZA WANAFUNZI WAKIFANYA UCHAFU ZAVUJA FACEBOOK SEE PHOTOS BELOW =>AdvertisementKAMA HUJAONAILE VIDEO CHAFU YA ZARI THE BOSS LADY ILIYOVUJA BOFYA HAPO CHINI=> Advertisement
Post a Comment