Almasi adimu duniani yagundulika Tanzania
Katika miaka karibu 250 ya historia ya minada, ni almasi tatu tu safi
za pinki zilizokuwa na uzito wa zaidi ya karati 10 zilizoonekana kwa
mauzo, kwa mujibu wa taasisi ya Christie’s.
KAMPUNI ya madini ya Petra Diamonds imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pinki yenye uzito wa karati 23.16 kutoka mgodi wake wa Williamson uliopo Mwadui, Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo ya madini, almasi hiyo ya pinki, moja ya madini ya rangi yanayosakwa zaidi duniani ni mfano wa ubora wa hali ya juu na ugunduzi mkubwa na muhimu zaidi kufanywa na Petra kutoka mgodi huo hadi sasa.

“Almasi za pinki hupatikana katika migodi michache duniani na uadimu
wake huzifanya kuwa moja ya madini yenye rangi yanayotafutwa zaidi
duniani,”taarifa ya kampuni hiyo ilisema.
Rangi ya pinki katika almasi inadhaniwa kuletwa kutokana na mabadiliko ya muundo wa molekuli, ambao unaaminika kusababishwa na aina fulani ya mtikisiko wa ardhi (seismic shock) unaotokea wakati wa kipindi cha uumbaji wa almasi.
Pande hilo la almasi litauzwa katika mnada huko Antwerp nchini Ubelgiji Desemba mwaka huu.
picha ikionyesha thamani ya dhahabu katika mpangilio wa rangi |
Post a Comment