MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AFARIKI DUNIA
TAARIFA
iliyotufijia hivi punde toka Wilaya ya Njombe mkoani Njombe zinaarifu
kua Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi Sara Dumba amefariki dunia hii leo aada
ya kuugua ghafla.

Marehemu
siku ya leo alikua kazini kama kawaida akitumikia taifa hadi.muda wa
jioni alipotoka na kurejea nyumbani kwa mapumziko na akiwa nyumbani hapo
ndipo alipoanza kuhisi afya yake kutetereka.
"Ni kweli
Mheshimiwa Sarah Dumba ametutoka, ni majonzi mazito na hadi sasa
siamini lakini huo ndio ukweli kua mwenzetu amefariki majira ya saa moja
usiku wa leo," kilisema chanzo chetu.
Sara Dumba amepata kuwa Mkuu wa Wilaya katika maeneo tofauti Ikiwepo Wilaya ya Kilindi na Njombe alikofikwa na mauti.
Father
Kidevu blog inatoa pole kwa familia yake, Wananchi wa Njombe, Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ofisi ya Waziri Mkuu
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia msiba huo mzito.
Taarifa kamili itawajia wakati wowote juu ya mipango ya mazishi.
Post a Comment