Loading...
Home »
Unlabelled »
MAKALA ; BAJETI 2016/2017
Advertisement
[1.5MB] download video ya LULU akiwa bafuni anaoga ==>
Advertisement
BAJETI CHUNGU KWA WANANCHI FUATILIA
HULKA
ya falsafa ni kudadisi, kuhoji na kushangaa na nia ikiwa kusaka ukweli
utakaowezesha kuondoa shaka katika jambo linaloonekana kuwa zito.
Nimekuwa nikiamini katika falsafa hiyo kwa muda sasa ambayo naamini
imeniwezesha kutambua mambo mengi sana ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Kwa kutumia falsafa hiyo hiyo ya kudadisi, kushangaa na kuhoji
nimejielekeza katika kusaka ukweli kuhusu ubora wa Bajeti ya 2016/17
iliyosomwa hivi karibuni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip
Mpango.
Baada ya kuipitia nimejiridhisha pasi na shaka kwamba nina kila
sababu ya kuhoji na kwa kushirikiana na wasomaji ili kubaini kama bajeti
hiyo ya Magufuli itakuwa mwarobaini wa maendeleo ya serikali yake
kutimiza ahadi ya kuwainua wananchi wa hali ya chini.
Sababu nyingine iliyonichagiza kutazama Bajeti ya serikali kwa kina
inatokana na ukweli kwamba ndiyo inayotoa taswira ya kukamilisha jambo
lolote ikiwemo muelekeo wa serikali.
Wale wanaoshabikia bajeti iliyosomwa hivi karibuni wengi wao naamini
watakuwa hawajatumia falsafa ya kudadisi na kuingia kwenye mkumbo wa
kushabikia kila jambo bila ya kutafakari kwa undani.
Kama wabunge wetu wangekuwa wanatafakari mambo kwa mapana yake
nakuweka vyama vyao kando na kuliweka taifa mbele naamini wasingekubali
kupitisha Bajeti hiyo ninayoshawishika kusema bila kumeza maneno kwamba
haifai kwa Tanzania tunayoitaka.
Kwanini haifai? Kwanza inakwenda kinyume na ndoto za Rais John
Magufuli za kutaka watu wa hali ya chini kuishi kama ‘malaika’ (maisha
mazuri) lakini kwa bajeti hii imewanyonga kwa kutumia kinyongeo
kinachoitwa kodi.
Simaanishi kwamba ni vibaya kulipa kodi lakini kwa serikali ya Dk.
Magufuli imejielekeza kuwabana watu wa hali ya chini kabisa kwa kuongeza
kodi katika huduma za fedha zinazotumiwa na watu masikini za M-Pesa,
Tigo Pesa, Airtel Money.
Kuongeza kodi kwa Kampuni za simu maumivu huja kwa watumiaji ambao
wengi wao ni masikini na watu wa hali ya kati, kwa kuwa pindi
wanapoongezewa na wao huwaongezea watumiaji gharama za huduma.
Tatizo jingine ninaloliona na limeanza kulalamikiwa na Halmashauri
mbalimbali ni hatua ya ukusanyaji wa kodi za majengo ambazo kwa muda
mrefu zimekuwa zikikusanywa na halmashauri, lakini sasa imeamuliwa
zikusanywe na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kupelekwa Hazina. Wakati wanafanya hivyo hawakutafakari kwamba wataathiri kwa kiasi
kikubwa mapato ya Halmashauri kwa sababu vyanzo vyake vikuu vya mapato
ni kodi hiyo.
Kama utaratibu huo utatumika kwa fedha kukusanywa Hazina ndipo
baadaye ziombwe kwa Maendeleo utacheleweshwa kama ambavyo inatokea kwa
ucheleweshaji wa fedha kutoka Serikali Kuu zinachelewa kupelekwa katika Halmashauri basi tusitegemee kuwa fedha za kodi ya majengo zitanufaisha tena Halmashauri.
Kama wangeona historia ya kuziachia Halmashauri wasingechukua uamuzi
huo kwa sababu wakati kodi hiyo ilipokuwa ikikusanywa na Halmashauri na
kuwasilishwa Wizara ya Ardhi ilikuwa vigumu kurejeshwa kwenye
Halmashauri. Kama itafanyika hivyo inaanisha kwamba Halmashauri zitashindwa kabisa kutoa huduma kwa wananchi wake.
Tatizo jingine ninaloliona katika bajeti hiyo ya 2016/17 ni hatua ya
serikali kuingiza kodi ya asilimia 5 ya kiinua mgongo cha wabunge wakati
ukweli ni kwamba itaanza kutumika baada ya ukomo wa muda wa Bunge, sasa
unajiuliza ni kwanini iingizwe kwenye bajeti, fedha ambayo haipo na
inatarajiwa kupatikana mwaka 2020.
Ili pato hilo liweze kutumika labda serikali ingetoa mwongozo wa kusema kwamba fedha hizo zilipwe katika mwaka huu wa fedha.
Kwa suala la Tanzania ya Viwanda ambayo imekuwa ikiimbwa na Rais
Magufuli ili kupunguza kama si kuondoa tatizo la ajira inaonyesha ni
ngumu kutekelezeka. Ili kukamilika kwa ndoto ya rais Magufuli ilitakiwa sekta ya viwanda
ilitarajiwa maendeleo ya viwanda na uzalishaji ikue kwa asilimia 11
wakati mafanikio ni ukuaji wa asilimia 6.6.
Bajeti imeshindwa kutueleza bayana ni kwa namna gani Tanzania itaweza
kufika kwenye uchumi wa kati wa viwanda, hakuna tunapoelezwa hatua
yoyote ya awali labda ya kuandaa maeneo ya kufanyia shughuli za
uzalishaji wa kuwezesha viwanda, lakini ninachokishuhudia ni maneno
matupu. Bajeti iliyopangwa imeendelea kutenga fedha nyingi za matumizi pamoja
na kujipambanua kubana matumizi katika bajeti hii inaonyesha matumizi
ya kawaida kuwa sh. 13,336,042,030,510. Wakati fedha za miradi ya maendeleo Sh. 10,511,945,288,575 pekee hivyo inamaanisha matumizi ni muhimu kuliko maendeleo.
Sitaki kuingia sana kwenye hesabu za kitabu cha Mapato ya Serikali
ambayo yanaonyesha ni Sh Trilioni 22.063, huku serikali ikipanga kutumia
kiasi cha Sh Trilioni 23.847 ambacho ni tofauti na mapato serikali
iliyopanga kukusanya na tofauti yake inaonyesha kuwa na nakisi kubwa ya
Sh. Trilioni 1.783.
Wakati tumejipangia ukuaji wa kilimo kuwa asilimia 6 kwa mwaka lakini sasa ukuaji ni asilimia 3.2 ambao ni wote kuanzia uhuru.
Suala jingine la kuhoji hapa ni kwamba kuna umuhimu gani wa kujenga
kiwanja kipya cha ndege cha Chato kinamsaada gani kiuchumi kwa masilahi
ya Watanzania wote? Kwanini hizo bilioni 2 zilizotengwa kwa ajili ya kuanza kufanyika
upembuzi yakinifu wa ujenzi huo zisielekezwe katika kukarabati viwanja
vilivyopo kwa sasa?.
Kwanini hata kabla ya mwaka mmoja wa Dk. Magufuli madarakani ajengewe kiwanja cha ndege wakati Mwalimu Julius Nyerere alikaa miaka25?
PICHA CHAFU ZA WANAFUNZI WAKIFANYA UCHAFU ZAVUJA FACEBOOK SEE PHOTOS BELOW =>Advertisement
KAMA HUJAONAILE VIDEO CHAFU YA ZARI THE BOSS LADY ILIYOVUJA BOFYA HAPO CHINI=>
Advertisement
Thursday, June 16, 2016
Post a Comment