Na hichi ndicho alichokieleza
Wakubwa habari za asubuhi.
I’m still licking my wounds, kama wasemavyo
Waingereza.
Pamoja na kwamba vumbi la uchaguzi wa jana
bado limetanda, naomba niseme yafuatayo juu
ya uzoefu wa hizi siku chache zilizopita.
1) Kuna wanaodai tulikosea kutokuangalia
gender balance ndio maana tumeshindwa.
Hapana.
Kosa letu sio kutokuzingatia jinsia. Kosa letu
kubwa na lisilosameheka ni kuwa chama kikuu
cha upinzani dhidi ya MaCCM. Na tumelifanya
kosa hilo tangu mwaka 2010.
Wenzetu wa CUF nao walishawahi kufanya kosa
hili kubwa miaka ya nyuma na mnakumbuka
yaliyowapata. Na NCCR Mageuzi kabla ya CUF.
2) Kosa letu la pili ni kuwa chama kikuu cha
upinzani lakini bila kuwa na nguvu ya kutosha
bungeni kuzuia njama za MaCCM ndani na nje
ya Bunge.
Ni hivi. Sisi wa UKAWA tupo 116, MaCCM yako
252 na bado wanajiongeza i.e. Salma Kikwete na
wengineo watokao Magogoni. Wao wana 70%,
sisi tuna 30% ukihesabu kila mtu aliyeko
bungeni.
Kwa balance hii hata tukifanyaje tutaonewa tu.
Na chochote tutakachopata itakuwa ni kwa
fadhila yao.
Kwa sababu ya balance hii, hawahitaji hata
kuheshimu sheria na kanuni za Bunge.
Kati ya Jumamosi na jana wamebadilisha sheria
na kanuni za uchaguzi kwa namna ambayo
inatisha.
In fact, hawakufuata chochote kilichoandikwa
kwenye Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge wa
EALA. Badala yake, walibadilisha kanuni kadri
mchezo ulivyokuwa unaendelea na kadri ya
mahitaji ya maslahi yao.
Kanuni inavipa vyama vya siasa haki ya kuweka
mgombea mmoja hadi watatu kwa kila nafasi
inayogombaniwa. Ndivyo tulivyofanya. Machoni
pao tulikosea sana.
Kwa practice ya Bunge letu, wagombea
wasiokuwa na mpinzani hupita bila kupingwa. Na
hii ndio sheria yetu ya uchaguzi hata nje ya
Bunge. Jana imebadilishwa.
Wagombea wa CUF walikuwa wanne kwenye
nafasi moja wakati kanuni zinasema maximum ni
wagombea watatu kwa nafasi moja.
Watatu kati ya hao hawakuwa na fomu za uteuzi
zilizosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF kama
ilivyotakiwa na kanuni. Bali, kwa kauli ya Katibu
wa Bunge na Msimamizi wa Uchaguzi, majina
yao yalitokea NEC.
NEC inahusikaje na uteuzi wa majina ndani ya
vyama, mimi sijaelewa bado.
Kura zilipigwa kwa utaratibu usiokuwepo kwenye
kanuni kabisa. Hakuna upigaji wa kura ya ndio
au hapana kwenye uchaguzi wa EALA. Lakini
wamepigia wagombea wetu au hapana.
Hakuna utaratibu wa wengine wanapigiwa kura
ya ndiyo tu lakini wengine wanapigiwa ndio au
hapana kwenye karatasi hiyo hiyo moja ya kura.
Jana wagombea saba wamepigiwa kura za ndio
tu, wawili wamepigiwa ndio au hapana.
Kanuni inasema usipochagua wagombea tisa
basi kura yako imeharibika. Jana wamepigia
kura wagombea saba tu na hakuna kura yoyote
iliyoharibika.
Kanuni inaelekeza kura kuwa ya siri lakini jana
usiku hakukuwa na kura yoyote ya siri.
Na mengine mengi.
Yote haya yanatokana na dominance ya MaCCM
bungeni. Na juu ya yote haya, ongezea la
Msimamizi wa Uchaguzi ambaye anajifanya ni
refa wa mchezo huu lakini kiuhalisia ni kocha wa
timu ya MaCCM.
Katika mazingira haya, je, watu hawa wataitisha
uchaguzi mwingine ili kujaza nafasi mbili za
CHADEMA zilizobaki???
Hili ni kwa wale wanaofikiria tukiongeza jina
moja au mawili basi shida itakwisha na MaCCM
yatatupatia nafasi zetu. Mimi sina jibu lake lakini
hisia zangu zinaniambia hii imetoka.
Nitaendelea wakati mwingine.
Post a Comment