WAFANYAKAZI ZAIDI YA 600 WA MACHIMBO YA MADINI YA TANZANITE (TANZANITE ONE) KUACHISHWA KAZI..... FUATILIA
KAMPUNI ya madini ya Tanzanite One imetoa likizo ya malipo kwa
wafanyakazi 635 kwa lengo la kujiweka sawa katika shughuli za uendeshaji
wa kampuni hiyo.
Wafanyakazi hao wamepewa likizo ya malipo kuanzia jana huku
mchakato wa kuwaachisha kazi baadhi ya wafanyakazi ukiendelea kwa
kuhusisha pande zote.
Modest alisema hakuna mfanyakazi atakayeachishwa bila ya kufuata
sheria na taratibu za kazi kwani uongozi umezingatia kila kitu na
kuwataka wafanyakazi kuacha kuwa na wasiwasi juu ya hilo.
Alisema mchakato wa kupunguza wafanyakazi umetokana na kampuni
kushindwa kujiendesha kutokana na kukosekana kwa uzalishaji kwa muda
mrefu na gharama za uendeshaji kuwa kubwa.
Naye Mwanasheria wa Tanzanite One, Kisaka Mnzava alisema
kuachishwa kazi kwa wafanyakazi kutafuata sheria zote za kazi na
zitasimamiwa na pande zote na hakuna mfanyakazi atayeachishwa bila
kufuata sheria za nchini.
Alisema kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi sio mchakato mgeni katika
kampuni hiyo kwani ulishafanyika na hakukuwa na malalamiko yoyote.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Tanzanite One, Daniel Hagay
alikiri kuwepo kwa mchakato wa kupunguza wafanyakazi, lakini alikuwa na
wasiwasi juu ya taratibu kukiukwa, hivyo kuutaka uongozi kukamilisha
kwanza taratibu za kuachisha wafanyakazi ili kila mfanyakazi
atayeachishwa awe na haki yake ya msingi.
Alisema mchakato mzima wa upunguzaji wa wafanyakazi utafuata
taratibu na sheria za kazi ikiwamo kushirikisha pande zote ikiwemo
Stamico, mwakilishi wa serikali kama mbia na viongozi wa wafanyakazi.
Alisema Sky Group imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu
tangu ichukue kitalu hicho C kilichokuwa kikimilikiwa na Tanzanite One
kutokana na kukosa uzalishaji kwa muda mrefu, lakini pia imekuwa na
madeni makubwa ya nyuma.
Post a Comment